Waziri wa Ardhi James Orengo alikamilisha kutoa ushahidi wake mbele ya Tume ya Cockar na ujumbe kuwa aliyekuwa waziri wa Fedha Amos Kimunya alikuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba uuzaji wa hoteli ya Grand Regency ulikuwa chini ya sheria. Hata hivyo wakili wa Kimunya, Githu Muigai aliibuka na madai kwamba Orengo alikuwa anatimisha njama yake ya kummaliza mteja wake ilhali alijua kwamba hakuwa na hatia yoyote.
Link to this comment:
All Comments (0)