Shirika la msalaba mwekundu limeanzisha shughuli za kununua mifugo kutoka kwa jamii za wafugaji haswa katika maeneo yaliyoathirika na ukame.Shirika hilo linawanunua mbuzi kwa shilingi elfu mbili badala ya shilingi mia sita, na mifugo hao wanapaniwa kutumiwa kama chakula cha msaada kwa wenyeji wa maeneo yaliyoathirika na baa la njaa. Shirika hilo linanuia kuwapunguzia wafugaji mzigo wa hasara utakaotokana na mifugo wao kufariki. Nalo eneo la Marsabit linaendelea kuripoti maafa zaidi haswa kwa mifugo, kutokana na ukosefu wa maji.
VISION 2012 HOW ABOUT WATER FOR ALL KENYANS BE4 V2030
labanjumah 1 year ago