Mahakama ya rufaa imesitisha ukaguzi wa mahakimu na majaji hadi pale kesi ya mwanafunzi wa sheria denis mogambi itakaposikizwa na kuamuliwa. Mogambi amewasilisha kesi mahakamani kulalamikia ukaguzi huo akisema shughuli hiyo haiwapi wahusika fursa ya kukataa rufaa kupinga uamuzi dhidi yao. Jaji emmanuel okubasu, alnashir visram na david maranga wameagiza kuwa kesi hiyo iskizwe na kuamuliwa badaa ya siku 21. Bodi hiyo ya ukaguzi iliundwa ili kutathmini iwapo majaji na mahakimu hao wanayo tajriba ya kutosha ya kuendelea kuwa afisini au la.
Link to this comment:
All Comments (0)