Added: 4 years ago
From: ramso007
Views: 134,808
Sort by time | Sort by thread (beta)

Link to this comment:

Share to:

All Comments (108)

Sign In or Sign Up now to post a comment!
  • I miss Afrika

  • LAKINI WAPI WAUME????? .... acheni Ushamba. learn to mix men and women freely in parties and happiness.

  • can someone tell me a bit about taarab and how it uses the swahili language to unify the swahili people? Any information on the links between taarab and swahili culture and nationalism would be great thanks!

  • very nice taarab love from somalia

  • jamani nasikia  rahaaaaaaaaaaaaaa, wanaoumwa namjiue, tenaaaaaaaaaaaa.....

  • nini tena?msumari huooooooooooo.hahah bongo si mchezo,kweli tambalare nimekubali

  • NAONA HAYA SANA NIKIONA KINA MAMA WAKI HINUA MATAKO JUU.....KWELI AFRIKA IMEBADILIKA

    kina mama katikeni kawaida mambo ya juu juu wajieni ndogo ndogo!

  • vipi kupendwa nyinyi mu umiye?

  • mziki powa kabisa !

  • eeehhh jamani nipe raha mtoto

  • wacha tu!! haki wimbo poa kweli, wewee! najiamini!

  • nipe raha mpenzi wangu na mie nikupe zangu wow! halooooooooo

  • muziki bomba bila shaka wapendeza

  • dah jamani kila kukicha mambo yanazidi kufaana Tanzania jamani munatuuwa tufanyeje ikiwa viuno ni hivyo tutakufa wote wabaki vipofu tu,haya nipe raha mpenzi

  • Ama kwa kiburi hicho, na akili iso pima

    Na maneno kochokocho, yasoambiwa tuwama

    Sioni kuna maficho, zahama imeandama

    Yule aliye na macho, Wala hambiwi tizama

  • Tangu mwanzo wa mjadala au "utesi" huu, wenye zao razini wanajua fika debe tupu liko wapi! Nami nalipandisha daraja na kusema si tupu bali ni shinda. Nalo "Debe shinda haliachi kutika".

  • Jamani KHAIRU 'LMAWAAHIBU AL-AQLI WA SHARRU 'MASWAAHIBU ALJAHLU maanake KARAMA AMA KIPAWA BORA ZAIDI KWA MWANADAMU NI KUWA NA AKILI NA BALAA AU MSIBA MKUBWA KWA MWANADAMU NI KUWA PITE. Tena JAWABU SAFII ASSUKUUT. Naufunga ukurasa huu. Shukran sana kwa kuwa umenifunza mengi.

  • Sijui niuite ungazija, uzanzibara, uzanzibari au utanzaniabara. Pengine ustaarabu wa kishirazi. Makubwa hayo! Twaambiwa "la'haullah", jamani mwajua manake? Mimi sijui. Nambie " la' haula wala Quwata illa----- Maliza mwenyewe.

  • Ustaarabu huo. Maashallah! Leo twafunzwa ustaarabu! Kongole! Kongole bwamkubwa ustaarabu wa visiwani huo!

  • Kaka mwambe afahamu, kwamba najuwa kutunga,

    Nishikapo kunudhumu, mizani vina hupanga,

    Hasanifu tungo tamu, rai vema hizipanga,

    Hoja ninavyoziwanga, sizifanyii papara.

  • Kama nudhuma najuwa, wala sikuanza jana, Mola menipa kipawa, menijaliya kunena, Hushukuru Mwenye Quwa, kwani wengine hawana, Namba na kuambizana, mema yaliyo na tija. Mwamba matayo sijawa, naichelea laana, Kusema yayiyokuwa, walau ya kutukana, Si vizuri natambuwa, kaulimbi kupanana, Namba na kuambizana, mema yayliyo na tija. Wawapi wenye muruwa, wasokosa kutajana?, Kote kote kichunguwa, hukosi dhabidhabina, Ela yataka kutuwa, kwa nyendo za kulingana, Namba na kuambizana, mema yaliyo na tija.
  • "Shushushu" sijazoeya, sidhani ni uungwana,

    Ela katika duniya, hayo twayapata sana,

    Hishima ndio twabiya, ya mtu alolingana,

    Haifai kubezana, ingawa waja twapenda.

  • Shushushu sijazoea, sidhani ni uungwana,

    Ela katika duniya, hayo twayapata sana,

    Hishima ndio twabiya, ya mtu alolingana,

    Haifai kubezana, ingawa waja twapenda.

  • Tungajitia pambani na kujifanya wajuzi, tuelewe fika kwamba "Miongoni mwa wajuao wapo wanaojua zaidi". Raha iliyoje kulumbana na mtu aalim! Raha iliyoje kufaidi busara kwa mtu anayetambuliwa kuwa na busara! Vinginevyo ni sawa na kucheza ngoma goya!

  • Chambilecho wavyele, lililo moyoni ulimi hujepa. Na mtu anapocheza na jibwa, litamsindikiza msikitini. Inapofika ya binadamu kujipurukusha na kujidai kwamba yeye ni Aalimu 'lghaibu hapo inampasa ajichunguze. Vinginevyo nachelea kufanya kufuru hapa. Jambo usilolijua ni usiku wa kiza.

  • Nipa raha ya maneno, yalopangika makini,

    Tamu yasiyo mfano, ya mwenye zake razini,

    Hata moja ja matano, yasongiya akilini,

    Nipa unganipa nini, ela nipa cha kufidi.

  • Lugha hii ni yetu sote. Iwe ni lahaja ya kiamu, kimtangata,kimvita au hata kingwana. Wasomi na malenga hujinakia kujifunza lahaja zinginezo. Malenga kama vile shaaban bin Robert na Hassan Maalim Mbega wameyadhihirisha haya kwa kina katika vitabu walivyotunga.

  • kakaz357 unayajua haya?

    Licha kifupa kifupi, hata nundu na kiuno,

    Haramu mtu hanipi, pamoja na ovu neno,

    Na kwamba sina sikopi, kukopa si matukano,

    Haya mambo kwa mfano, ela si mimi na wewe.

    Raha ya Kiswahili hiyo!!!!

  • Kwamba chambile twambiwa, geuze kisha ulole

    Kwa makini twatungiwa, mishororo tele tele

    Fani za kisawasawa, na maneno pole pole

    Maneno yakuzinduwa, si mikuki na mishale.

    ahsanta buashraf

  • Muyaka ametwambia:

    Dunia mti mkavu, kiumbe siulemele,

    Ukaufanyia nguvu, kuudhibiti kwa ndole,

    Mtiwe ni mtakavu, mara ulikwangushile,

    Usione kwenda mbele, kurudi nyuma si kazi!

    Gwiji wa Mvita huyo!!!!

  • Kaka mwambe afahamu, kwamba najuwa kutunga,

    Nishikapo kunudhumu, mizani vina hupanga,

    Hasanifu tungo tamu, rai vema hizipanga,

    Hoja ninavyoziwanga, sizifanyii papara.

  • Kaka mwambe afahamu, kwamba najuwa kutunga,

    Nishikapo kunudhumu, mizani vina hupanga,

    Hasanifu tungo tamu, rai vema hizipanga,

    Hoja ninavyoziwanga, sizifanyii papara.

  • Kaka mwambe afahamu, kwamba najuwa kutunga,

    Nishikapo kunudhumu, mizani vina hupanga,

    Hasanifu tungo tamu, rai vema hizipanga,

    Hoja ninavyoziwanga, sizifanyii papara.

  • Mafuta sijayaona, na maji yakiungana,

    Vovote tungakazana, ni huja iso maana,

    Jambo lisowezekana, viwi kulishika sana,

    Muhali kutangamana, lila na fila twambiwa.

  • Kiburi ni vazi la Mwenyezi Mungu. Iweje niambiwe kwamba nina kiburi? Mwenye macho haambiwi tazama. Wanaosoma haya tunayoyaandika hapa wanajua fika nani anayetakabari. Wala Mwenyezi Mungu asinijaaliye kuwa na kiburi yakanifika yaliyomfika ibilisi, imamu wa ufasiki.

  • Ninaposema wasomi wa Kiswahili, sina maana ya hao walio na shahada za vyuo vikuu pekee. Kuna Sheikh Ahmad Sheikh Nabhany, gwiji wa Kiswahili kutoka Lamu, Kuna Ustadh Haji Gora wa Unguja, watu kama vile Marehemu Saidi Karama, Marehemu Ali Salim Kibao wa Tanga na Mzee Hamisi Akida. Wote hao ni Waswahili. Wazungu wote niliyokutana nao na ambao wametafiti mas-ala ya Kiswahili nchini Kenya, walimshauri kwa kiasi kikubwa mzee wetu Ahmad Nabhany. Bora kwambizana ukweli. Waswahili halisi wanajulikana.

  • Kamusi ya kwanza ya Kiswahili iliandaliwa na Ludwig Krapf na ilikuwa katika lahaja za kaskazini. William Taylor, Stigand, Whiteley na Harries waliandika mambo mengi kuhusu lahaja za kaskazini. Kiunguja kiliteuliwa kuwa Kiswahili sanifu kwa sadfa. Baadhi ya wanakamati walipendekeza Kimvita kwa sababu kilikuwa na maandishi mengi. Kiswahili kinachosemwa katika Pwani ya Afrika Mashariki ndicho Kiswahili halisi. Mengine tuyasemayo ni porojo za pesa nane.

  • Hakuna swifa nzuri kwa binadamu kama kuwa mkweli. Asili ya Kiswahili ni pwani ya Afrika Mashariki. Wasomi wengi wanasema kwamba yamkini asili ya kiswahili ni Pate, Siyu na Lamu. Tangu Mrima hata Mvita, wazee wetu wakinena kwamba uswahilini ni kaskazini. Kuna mashairi mengi ya karne zilizopita yanayoashiria hoja hii. Pia dhana ya "waswahili" ingali ikiwatatiza baadhi ya watu. Asili ya neno "Swahili" ni kizungumkuti kwa watu wengi.

  • Hakuna swifa nzuri kwa binadamu kama kuwa mkweli. Asili ya Kiswahili na pwani ya Afrika Mashariki. Wasomi wengi wanasema kwamba yamkini asili ya kiswahili ni Pate, Siyu na Lamu. Tangu Mrima hata Mvita, wazee wetu wakinena kwamba uswahili ni kaskazini. Kuna mashairi mengi ya karne zilizopita yanayoashiria hoja hii. Pia dhana ya "waswahili" ingali ikiwatatiza baadhi ya watu.

  • Mintarafu mapisi ya Kiswahili, wazungu walipata kufahamu kuwako Kiswahili kutokana na maandishi mengi ya Kiswahili ya Lamu na Mombasa. Kina Ali Koti, Muyaka, Mwalimu Sikujua, Sayyid Nassir (mwenye Inkishafi). Kwa hivyo ukweli unajulikana kwamba Kiswahili kimetambulika kimataifa dhamana na washairi wakongwe wa pwani ya Kenya. Quli lhaqqa wa in kaana muran twaambiwa.

  • Haijambo kuliziba ua kwa ungo hata kwa peku mtu akitaka. Lakini vyereje kwa mtu anyeliziba jua kwa kitanga cha mkono? Si makubwa hayo? Na vipi huyo tumbiri anayejiziba uso na kukaa akifikiri kajiziba mwili mzima? Au huyo mbuni anayefutika kitwa chake ardhini akajitia hamnazo akidhani kwamba mwili wake mzima umefutikwa ardhini?

  • Shushuuy naona haufamu natija ya lahaja katika kiswahili. Kama mpenzi wa kiswahili nakuomba ufanye utafiti wa lahaja za kiswahili. Itakutoa matongo! jiulize ni pesa, senti, darahima,shilingi ama hela ?

  • Ustadh Amiri A.S.(Sauti ya Kiza) katika shairi lake la KUTENDANA anasema,

    Nipa na mimi nikupe, kupana ni kupeana,

    Leo nasema kweupe, si usiku ni mchana,

    Ni kwa vyangu unenepe, hutaki kugawizana,

    Nyege ni kunyegezana, nyegeza nikunyegeze.

    Nyegeza nikunyegeze, nyege ni kunyegazana,

    Wataka nikunoneze, hutaki kunonezana,

    Nikisema nipuuze, vipi mwanzangu wanuna!

    Gawa ni kugawiana, gawa na mimi nigawe.

  • shairi zuri sana hili. Ahsanta mwenzangu.Ela sikujua mada yangu italeta kutoelewana hivi. Hata hivyo nanufaika na mashairi na mawazo uliyotoa. Hongera.

  • Shukran Jaziilan. Nimejifunza mengi pia. Sidhani kuna farka yoyote iliyojitokeza. Wala sijalitwaa jambo hili kwa uzito unaovyaza khasama.

  • KHAIRU 'LMAWAAHIBU AL-AQLI WA SHARRU 'MASWAAHIBU ALJAHLU maanake KARAMA AMA KIPAWA BORA ZAIDI KWA MWANADAMU NI KUWA NA AKILI NA BALAA AU MSIBA MKUBWA KWA MWANADAMU NI KUWA PITE. Asiye na sikio akaazime!

  • Wajua unanishangaza na ninakuomba kwa hisani yako tuache masihara. Niwe mwalimu nisiwe mwalimu inahusianaje na mada ya NIPA na NIPE? Ukenya na Utanzania unaingilia wapi? Hivi twashindana kuonyeshana wanaojua na wasiojua Kiswahili? Kwa hisani yako tutumie lugha ya heshima. Chambilecho wazee wetu "HESHIMA SI UTUMWA". Nakuachia kauli hiyo! Na tena nakwambia "umenishinda" kwa yako uliyosema kwa hivyo hakuna haja ya kujadiliana tena. Wewe ni bingwa! Ma'a ssalaama!

  • KHAIRU 'LMAWAAHIBU AL-AQLI WA SHARRU 'MASWAAHIBU ALJAHLU maanake KARAMA AMA KIPAWA BORA ZAIDI KWA MWANADAMU NI KUWA NA AQLI NA BALAA AU MSIBA MKUBWA KWA MWANADAMU NI KUWA PITE. Asiye na sikio akaazime!

  • Maashallah! TZ nije kwambiwa LAMAZANI na LAZI. Ukisema Zanzibar na Pemba nitakuelewa. Tena nakuona wewe ni msomi maridhawa wa kuweka takwimu na kujua kwamba zaidi ya watu asilimia 70 hawajui Kiswahili nchini Kenya. Ulijuaje? Una ushahidi gani? Na wewe njoo Mombasa, Lamu na Malindi ujionee mwenyewe. Sina haja ya kuja kuboronga Kiswahili changu

  • Ah mwenzangu yanini zahama? Hebu na sisi tujivunie mila na desturi zetu. Utamaduni wa kiswahili ni wetu, uwe umetoka Lamu, Unguja Pemba hata Congo....ili mradi lugha ni ya kiswahili. Lahaja zetu ni urithi wetu

  • Kanama pana uzito, kwamba asoambilika,

    Akheri awe mtoto, atakaye kulimka,

    Kwa mkubwa si matoto, utasema utachoka,

    Vyereje mtu na mato, ela huiza kuona?

  • Sioni faida ya mjadala unaoelekea kuumbuana. Hakuna anayebwaka wala kuropoka. Mambo kuelemishana wala si kuonyeshana ujuzi. Kushindana kusikokuwa na tija hakufai pesa mbili. Yakifika hapo sina la kutenda ila kupiga horomo.

  • Sioni faida ya mjadala unaoelekea kuumbuana. Hakuna anayebwaka wala kuropoka. Mambo kuelemishana wala si kuonyeshana ujuzi. Kushindana kusikokuwa na tija hakufai pesa mbili. Yakifika hapo sina la kutenda ila kupiga horomo.

  • Mwenzio mimi sijifanyi hodari kwa kuwa najua kuna mabingwa zaidi yangu mimi. Kuna watu ambao mimi sienui ulimi wangu mbele yao, na hata kama nitasema nasema jambo nililo na hakika nalo. Mpaka sasa sijawahi "kujipiga chenga" na InshaAllah huko twendako "sitajipiga chenga".

  • Vipi nitajipiga chenga? Fani niipendayo zaidi katika Kiswahili ni huo ushairi. Niseme hiyo ndiyo raha yangu tangu zamani. Fani nyingine ninazipenda lakini hakuna inayoipiku fani ya ushairi. Hasa mashairi ya karne zilizopita.

  • Sijacharuka lolote! Ni mtu na zangu timamu ila natekeleza amali niipendayo. Maanake si maneno matupu! Wala sikuyaanza leo. Nakushukuru sana kwa kuwa hoja zako zimechochea ilhamu yangu ya utunzi hadi ya kupata beti mbili tatu!

  • Hivi ulijua vipi kwamba mimi mtunzi

  • Vipi nisijue? Ninajua tena najua sana. Wakumbuka Garissa?

  • salam alekum tena ndugu yangu. Kweli hapo umepata. nakukumbusha shairi lako mwenyewe

    lasema ulumbi si matukano dawa ya fumbo fumbuzi

  • Waaleykum ssalaam. Siku zote "Ulumbi si matukano, dawa ya fumbo fumbuzi". Lakini hayo kwa mwenye zake razini. Vinginevyo itakuwa maneno matupu yasiyokuwa na tija wa faida.

  • Kuna washika matayo, kama mwana na mbeleko,

    Wanayoyanena siyo, hayana kina na mbeko,

    Walong'ata yayo hayo, huona wendo maduko,

    Kufyoana mimi siko, ulumbi una nidhamu.

  • Langu jicho nakodowa, naola munayosema

    Hoja munazozittowa, mimi hapa nazipima Siwashi kisha ngazima.

    Upo buashraf

  • Huyu bwana anatoka Unguja kwa hivyo kama kwao hawasemi "nipa" itakuwa makosa kwangu kumtarajia aseme hivyo. Tena mimi sikusema kwamba kusema "nipe" ni makosa. La hasha! Wewe ndiye unayepinga matumizi ya "nipa"! Nami kwa kuwa mambo ni kutanabahishana nimejaribu kukuthibitishia kwamba "nipa" ni Kiswahili.

  • Mbwene mtu kupingana, kanama nimedangana,

    Kanamba "nipa" hapana, eti si sawa kunena,

    Najua kuna "kupana", ela twamba "kupeana".

    Tumeshika "kupeana", tukaliwaa "kupana",

    "Pea" na hiyo "peana", kwengine "kufagiana",

    Mtu angamba "panana", leo neno geni sana.

  • Waamu na wamvita, nduzangu nipulikani, Kuna swala lenye tata, ndilo nawaulizeni, Nambe "nipa" tukateta, hambwa hayo ni mageni, Naomba jibu nipani, kwamba "nipa" ni makosa? Wavyele nilivopata, wachamba sana "nipani", Mabingwa tulowafata, watumie lugha hini, Leo mtu amepita, amba haiwezekani, Naomba jibu nipani, kwamba "nipa" ni makosa? Sijui wamtang'ata, ela hao wabajuni, Nipa hawajaiata, waambe tangu zamani, Kuinena sitosita, madamu naiamini, Ningawambia nipani, wala sioni makosa.
  • Nipa na nikupe ni mambo mbali mbali. Kamwe huwezi kusema "nikupa" ila ikiwa umelenga kulinganisha vina mathalani katika shairi. "ku" iliyo kati inabadilisha mambo kwa kuwa hiyo "ku" ni kiambishi cha "wewe". Kuna "kupawa" ambako ni sawa na "kupewa". Kuna "kupana" ambako siku hizi watu husema "kupeana". Nadhani itakuwa kichekesho kwako pia kusikia "kupanana".

  • Mbona Bhalo hakusema "nduyangu nipe la kweli"? Waamu husema "mbwa nyani", unajua maanake? Kwa kuwa Pemba, Dar, na Unguja hawasemi hivyo basi hicho si Kiswahili? Kiswahili ni nini? Nana Mwanakupona anasema katika utenzi wake maarufu, NEGEMA WANGU BINTI kwa nini hakusema NEGEME WANGU BINTI maanake NIEGEME BINTI YANGU?

  • Na je hiyo NIPA LOHO YA KIHINDI? Ukweli ninaousema ni huo kwamba NIPA husemwa na waamu, wapate, wasiu na wamvita. Sema vijana tu ndio wameingia kwenye hayo maskuli yetu wakafunza "hicho Kiswahili sanifu"! Kwamba Dar, Pemba na kote ulikokutaja hawasemi hivyo haiwi sababu kwamba si kiswahili. Kwani waamu, wamvita, wasiu nk si waswahili? Nenda Lamu, Siu, Pate au Kiunga utasikia mengine mengi ambayo ndugu yangu utasema si Kiswahili!

  • Nipa loho ya kihindi

    wino na kalamu kandi

    nikuswifie mapendi.

    Yameningia moyoni

    kwa sahihi ya aini

    kana wanja wa machoni.

    'Takutunza uje kwangu

    kana wa kwanza mwanangu

    yako si nusu wa yangu

  • Na je hiyo NIPA LOHO YA KIHINDI? Ukweli ninaousema ni huo kwamba NIPA husemwa na waamu, wapate, wasiu na wamvita. Sema vijana tu ndio wameingia kwenye hayo maskuli yetu yakafunza "hicho Kiswahili sanifu"! Kwamba Dar, Pemba na kote ulikokutaja hawasemi hivyo haiwi sababu kwamba si kiswahili. Kwani waamu, wamvita, wasiu nk si waswahili?

  • Nimepata kibao cha Juma Bhalo. Tazama "bhalo - kweli mahaba udhia" hapa katika Youtube. Ukikisikiliza kibao hicho utapata "NIPA" katika dakika ya (02:47) ambapo Bhalo anasema "nduyangu nipa la kweli"

  • Nimepata kibao cha Juma Bhalo. Tazama "bhalo - kweli mahaba udhia" hapa katika Youtube. Ukikisikiliza kibao hicho utapata "NIPA" katika dakika ya (02:27) ambapo Bhalo anasema "nduyangu nipa la kweli"

  • Nimeshakupa kibao cha Bhalo na mwenyewe umemsikia anavyosema. Hoja ya Kiswahili sanifu imezungumzwa kwa muda mrefu na waliotutangulia kwa hivyo hata tukaizungumzia hapa hatufaidi lolote. Ukiufuata usemi wangu vizuri nimesema tangu hapo "hicho kiitwacho Kiswahili sanifu". Hii ni hoja ambayo ina siasa chungu mbovu na hatutamaliza tukiuanza mjadala.

  • Shushuuy sijui kama wewe ni shabiki wa muziki wa taarabu kutoka mwambao wa Kenya. Mara nyingi utawasikia watiribu wakisema "nambiani" au "pulikani" badala ya nambieni au pulikeni ambayo ni "sawa" mintarafu hicho Kiswahili sanifu.

  • Kusema hakika katika lahaja za kaskazini wengi husema "nipa". Ukimsikia asemaye "nipe" huyo kaathiriwa na Kiswahili sanifu. Wala si makosa kwao kusema hivyo kwa sababu ndicho Kiswahili walichokizoea. Maanake hiyo herufi "e" husalia "a". Kaskazini hawasemi LETE wanasema LETA!

  • Katika kimvita na kiamu ama tuseme lahaja za kiswahili za kaskazini mtu kusema nipa kwa maana ya nipe ni jambo la kawaida. Si hasha kumsikia mtu pia akisema "Nisalimiya nyumbani" kwa maana ya "Nisalimiye (jamaa) nyumbani". Haya ni nadra kupatikana katika hicho kiitwacho "Kiswahili sanifu"!

  • Langu sikio tu! hehehe. nipa raha au nipe raha!? waswahili mpo

  • Nipa na nipe yote ni mamoja! Pengine asiyejua atakwambia vingine. Waswahili halisi hayo wayajua sana. Bila shaka Kakaz najua hayo nawe wayajua! Upo lakini! Kwenu mmetuzidi na nini?

  • Kakaz357 uko wapi? Umeuwasha moto kisha ukatoweka?

    Ebu nikupe vitu hapa! Pengine vitakukumbusha enzi hizo!!! Wajua sana! Je bado unayashughulikia haya?

    Kuna washika matayo, kama mwana na mbeleko, Wanayoyatunga siyo, hayana kina na mbeko, Walong'ata yayo hayo, huona wendo maduko, Kufyoana mimi siko, ulumbi una nidhamu.

  • Kakaz357 uko wapi? Umeuwasha moto kisha ukatoweka?

    Ebu nikupe vitu hapa! Pengine vitakukumbusha enzi hizo!!! Wajua sana! Je bado unayashughulikia haya?

    Kuna washika matayo, kama mwana na mbeleko, Wanayoyatunga siyo, hayana kina na mbeko, Walong'ata yayo hayo, huona wendo maduko, Kufyoana mimi siko, ulumbi una nidhamu.

  • Fumbo mfumbie mjinga mwerevu atang'amua. Ebu nambieni nani huyo anayefyolewa na Mzee bin Yusuf? Nadhani naipatapata. Mwamwona binti anayesifiwa? Kuna jambo hapa!

  • nice clip

Loading...
Alert icon
0 / 00Unsaved Playlist Return to active list
    1. Your queue is empty. Add videos to your queue using this button:
      or sign in to load a different list.
    Loading...Loading...Saving...
    • Clear all videos from this list
    • Learn more